Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Taifa la Tanzania na Balozi Togolani Idriss Mavura mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezungumza na Flora Nducha kuhusu suala hili muhimu.“Nataka niwe mkweli; hii ni moja ya changamoto zetu kubwa zaidi. Hatuwezi kufanya kazi hii kama wale wanaojaribu kusaidia wanazuiwa kufanya hivyo, au kuwekwa katika hatari.” Ni sehemu ya barua ya Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, aliyowaandikia wananchi wa Jamhuri ya Kidemorkasia ya Congo, DRC wakati huu vikwazo kama vile mapigano jimboni Ituri, yanakwamisha harakati za kudhibiti mlipuko wa 17 wa Ebola nchini humo.Vikwazo vingine vya kudhibiti Ebola nchini DRC ni mila. Maki Baraka mkazi wa Beni jimboni Kivu Kaskazini ambako Ebola imeripotiwa mji jirani wa Butembo ana wito.Na Joyce Msuya, Naibu Mkuu wa Ofisi ya UN inayoratibu misaada ya dharura, OCHA anatamatisha jukumu lake baada ya kuhudumu kwa miaka minne. Anold Kayanda amemuuliza anachokumbuka zaidi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör United Nations. Innehållet i podden är skapat av United Nations och inte av, eller tillsammans med, Poddtoppen.