Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalumu ambapo hii leo tutaelekea jijini Kampala nhcini Uganda kuangazia uzunduzi wa awamu ya tatu ya safari ya hija ya “Twende Zetu Butiama”, kumuenzi Hayati Mwalimu Julius Kmabarage Nyerere, rais wa zamani wa Tanzania aliyedumisha amani, msikamano na kupigania maendeleo ambazo ni ajenda zinazopewa kiaumbele cha juu na Umoja wa Mataifa. Shuhuda wetu katika uzinduzi huo uliofayika mwishoni mwa wiki alikuwa ni John Kibego kutoka Radio washirika wetu Kazi Njema FM ya mjini Hoima.Tukianza na ugonjwa wa Ebola lakini leo ni habari njema, wauguzi wanne waliokuwa wamelazwa hospitalini huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC wameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupona ugonjwa huo, na kufanya idadi ya waliopona virusi vya Ebola hadi sasa kufikia watu watano. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya Duniani WHO katika taarifa yake limesema “Tunatarajia kuona watu zaidi wakipona, hasa wale wanaogunduliwa mapema na kupata huduma za afya kwa wakati, huku juhudi za kudhibiti mlipuko zikiongezwa kasi.”.’Kamati ya haki za watoto ya Umoja wa Mataifa imelaani sheria iliyopitishwa na uongozi wa Taliban nchini Afghanistan ya kuwa mtoto wa kike akisha balehe tu tayari anaweza kuolewa. Kamati imesema sheria hiyo mpya ni ukiukwaji mkubwa na wakimfumo wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na kwamba Taliban wanachukulia ukimya wa wasichana kama ridhaa, na kwamba amri hiyo ni muendelezo wa mfululizo wa hatua za kibaguzi zinazochukuliwa na utawala wa Taliban,".Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, hii leo ameonya kuwa kuenea na kuhamishwa kwa njia haramu kwa silaha ndogo ndogo na nyepesi kunaendelea kuchochea migogoro, ugaidi, uhalifu na ukatili wa kijinsia duniani kote, huku akizitaka nchi kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na vitisho vinavyoibuka.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör United Nations. Innehållet i podden är skapat av United Nations och inte av, eller tillsammans med, Poddtoppen.