Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Jamhuri ya Kidokrasia ya Congo DRC katika mji wa Mavivi jimboni kivu kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kusikia ni kwa jinsi gani walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya MONUSCO. wanavyochangia katika ulinzi wa amani na msaada wa kibinadamu.Umoja wa Mataifa umezitaka nchi zote duniani kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema baada ya kuthibitisha kuanza kwa hali ya El Niño, ukionya kuwa mabadiliko hayo ya joto la Bahari ya Pasifiki yataleta viwango vya juu vya joto kuliko kawaida karibu kila mahali duniani kati ya mwezi Juni mpaka Agosti na kuchochea matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa duniani WMO, Celeste Saulo amesema "Taarifa hizi ni muhimu kwa sababu El Niño ni kichocheo kikubwa cha hali ya hewa duniani na mifumo ya mabadiliko ya tabianchi, bahari yenye joto, huongeza joto na unyevu kwenye mfumo wa hali ya hewa ambao unaweza kutumika kuzidisha hali mbaya ya hewa ikiwa ni pamoja na joto kali, na mvua kubwa.”.’Zinakaribia siku 100 sasa tangu kuanza kwa mzozo wa Mashariki ya Kati ambao athari zake zimesambaa duniani kote kwani umevuruga njia za usafirishaji na umeongeza gharama za usafiri na kuchelewesha utoaji wa huduma muhimu. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limeeleza kuwa fedha nyingi sasa zinatumika kwenye usafirishaji badala ya kununua vifaa vya kuokoa maisha ya watoto. Gharama za kusafirisha chanjo kwenda baadhi ya nchi barani Afrika zimeongezeka kwa hadi asilimia 70, huku gharama za kusafirisha chakula tiba, na vifaa vya elimu, nazo zikipanda kwa kiwango kikubwa. Shirika hilo linaonya kuwa hali hiyo inalazimisha kufanya maamuzi magumu kuhusu ni watoto gani wapate msaada kwanza". Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliogundulika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC na Uganda mwezi uliopita wa Mei ambapo mpaka sasa watu 49 wamepoteza maisha, 48 nchini DRC na mmoja nchini Uganda. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amezihimiza jumuiya za kimataifa kutoa usaidizi unaohitajika ili kudhibiti mlipuko. Pia amelihimiza nchi kutoweka vikwazo vya usafiri kwa DRC, ili kuhakikisha msaada wa kiafya na kibinadamu unaweza kufikia kiwango kinachohitajika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "CHOTORA"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör United Nations. Innehållet i podden är skapat av United Nations och inte av, eller tillsammans med, Poddtoppen.