Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zimezindua Siku ya Ziwa Victoria ambayo maadhimisho yake kwa mara ya kwanza yamefanyika tarehe 21 mwezi huu wa Mei huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Lengo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha vivutio vya utalii. Uzinduzi huu ulitanguliwa na jukwaa la wadau wa Bonde la Ziwa hilo lililohudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Amon Manyama, Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania. Rashid Malekela wa Idhaa hii alituwakilisha na amezungumza naye.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno kama neno "PEKEPEKE."Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa UNCERF umetoa dola milioni 60 kusaidia muitikio wa kupambana na ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC. Tayari vifaa tiba vimewasilishwa nchini humo na sasa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO na wadau wengine wanaendelea na usaidizi ikiwemo kuweka vituo vya kuimarisha hatua za kuzuia maambukizi na kuhakikisha utunzaji salama wa wagonjwa..Mwakilishi wa mpya wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Togolani Mavura amewasilisha rasmi nyaraka zake kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jijini New York Marekani na kueleza yale aliyokuja nayo.shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema fedha zinazotumwa nyumbani na watu waishio ughaibuni au diaspora sasa zimezidi kiwango cha fedha za misaada rasmi ya maendeleo na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje. IOM imeeleza pia namna diaspora walivyo na msaada mkubwa wakati wa majanga kwa kutuma fedha haraka, huduma na usaidizi kupitia mitandao ya kuaminika katika nchi mbalimbali ikiwemo Somalia, Haiti, Ufilipino na Ukraine.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör
United Nations. Innehållet i podden är skapat av United Nations och inte av,
eller tillsammans med, Poddtoppen.