Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania Kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambako Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inaendelea kuwa mfano wa jinsi binadamu, wanyamapori na urithi wa kitamaduni vinavyoweza kuishi pamoja huku vikichangia maendeleo ya utalii endelevu na ulinzi wa mazingira. Je nini kinafanyika kuhakikisha uhifadhi, utamaduni, mazingira na utalii vinakutana kwa mustakabali endelevu? Ili kupata majawabu Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na Kamishna wa Hifadhi ya Ngorongoro, Abdul-Razaq Badru.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameendelea kusisitiza umuhimu wa ugunduzi wa mapema kwani hatua zikichukuliwa haraka wagonjwa wa Ebola wanapona. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Geneva Usiswi baada kurejea kutoka ziarani mashariki mwa DRC amesema, Kufikia sasa, watu sita wamepona nchini DRC na wawili nchini Uganda, jambo linaloonesha kuwa watu wanaweza kupona Ebola iwapo watapata huduma za afya na kwenda vituo vya afya mara tu wanapoanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo.Kuelekea kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la FIFA wiki ijayo hapa Marekani na katika nchi jirani, Canada na Mexico, Shirika la Afya la Nchi za Amerika (PAHO) limetoa wito kwa nchi za bara la Amerika kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa wa surua na Rubella kufuatia mikusanyiko mikubwa inayotarajiwa na milipuko inayoendelea ya surua na ongezeko la safari za kimataifa vinaweza kuongeza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo. Shirika hilo linazitaka mamlaka za afya kubaini maeneo yaliyo katika hatari kubwa na kuimarisha hatua za kukabiliana haraka ili kuzuia maambukizi zaidi. Na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa asubuhi hii kwa saa za New York, Marekani wanachagua wanachama watano wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe 1 Januari 2027 hadi 31 Desemba 2028. Kutoka Barani Afrika mgombea mmoja ni Zimbabwe ambaye hata hivyo anatarajiwa kupita kwani hana mpinzani katika nafasi hiyo. Nchi zitakazochaguliwa zinachukua nafasi za Somalia, Pakistan, Panama, Denmark na Ugiriki, ambazo mihula yao itaisha mwishoni mwa mwaka huu 2026.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör
United Nations. Innehållet i podden är skapat av United Nations och inte av,
eller tillsammans med, Poddtoppen.