MAELEZO PODCASTS
Avsnitt

Miaka 10 ya BMH: Jinsi Hospitali ya Benjamin Mkapa Ilivyobadilisha Huduma za Kibingwa Tanzania

Dela

Hospitali ya Benjamin Mkapa ni hospitali ya rufaa ya kanda iliyopo jijini Dodoma, iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa huduma za kibingwa ambazo kwa sasa zipo 20 na ubingwa bobezi zipo 17 kwa wananchi wa Tanzania na nchi jirani. 


Tangu kuanza kutoa huduma zake, hospitali hiyo imeendelea kukua kwa kasi na kuwa miongoni mwa vituo vinavyoongoza nchini katika huduma za matibabu ya moyo, figo, saratani, upasuaji mkubwa pamoja na huduma za kisasa za uchujaji damu na upandikizaji wa figo. Aidha, hospitali imejizatiti katika kukuza utalii wa matibabu na mafunzo ya kitaalamu, huku ikitoa huduma kwa mamilioni ya wananchi kila mwaka. 

Support the show

Msemaji Mkuu wa Serikali

Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör Tanzania Information Services Department (Idara ya Habari-MAELEZO). Innehållet i podden är skapat av Tanzania Information Services Department (Idara ya Habari-MAELEZO) och inte av, eller tillsammans med, Poddtoppen.