Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu na vijana kuhusu siku ya amani, ufunguzi wa UNGA81, Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni.

• Leo ni siku ya amani duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amepongeza watu wote mashinani wakiwemo watumishi wa kujitolea, wachechemuzi na viongozi wa mashirika ya kiraia wanaojitolea kwa hali na mali kuendeleza amani. • Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataofa UNGA81 unafungua pazia kesho Jumanne ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa kwa kina na nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa ikiwemo kuwasilisha tarifa zao • Kesho Jumanne tarehe 22 Septemba mbali ya kufunguliwa kwa mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Matanfa wa UNGA81, kandoni mwa mjadala huo kutakuwa na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni. Balozi Philip Thigo anayehusika na masuala ya AI kutoka Kenya ni miongoni mwa watakaoshiriki mkutano huo amenieleza kwa nini suala hili ni muhimu katika mkutano wa kesho na nini wanakitarajia. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör United Nations. Innehållet i podden är skapat av United Nations och inte av, eller tillsammans med, Poddtoppen.