Hii leo jaridani tunaangazia uokoaji Gaza baada ya jengo moja kuporomoka na kuwanasa watu chini ya vifusi, ushirikiano na Umoja wa Mataifa, na chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi nchini Burundi.
• Hofu na majonzi vimetanda Gaza baada ya jengo moja kuporomoka na kuwanasa watu chini ya vifusi. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 100, wakiwemo watoto 50, walikuwa wakiishi katika jengo hilo wakati lilipoanguka. Operesheni za uokoaji zinaendelea, huku Umoja wa Mataifa ukisema kila dakika ni muhimu katika kujaribu kuokoa maisha.
• Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya kuhusu kuongezeka kwa vitisho, kulipiza visasi na ufuatiliaji wa kidijitali unaovuka mipaka dhidi ya watu na wadau yanayoshirikiana na mfumo wake unaohusiana na masuala ya haki za binadamu. Kufahamu kwa kina kilichomo kwenye ripoti hyo nimezungumza na Selina Jerobon ambaye amefuatilia kwa kina.
• Hivi karibuni, Burundi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, pamoja na wadau wengine, imezindua mpango wa chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, mpango unaolenga kuwachanja wasichana wenye umri wa miaka tisa hadi 14
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör
United Nations. Innehållet i podden är skapat av United Nations och inte av,
eller tillsammans med, Poddtoppen.