Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DR Congo kufuatilia mapambano dhidi ya ebola ambayo yameanza kupata matumaini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.
• Mlipuko wa sasa wa 17 wa Ebola wa virusi vya Bundibugyo huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umegharimu zaidi wanawake na wasicha kwa kuwa wengi wao wako mstari wa mbele kuhudumia wagonjwa na familia zao licha ya hatari kubwa ya kuambukizwa. Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva, Uswisi, kwa njia ya mtandao kutoka Kinshasa DRC, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake, (UN Women) nchini humo, Dkt. Setcheme Mongbo, amesema. “Wanawake na wasichana huosha miili ya marehemu na kushiriki katika shughuli nyingine za mazishi, wao ndio wanaokusanya na kutoa maji na chakula kwa wanafamilia. Na suala la utoaji wa huduma hizo ni muhimu sana katika mnyororo mzima wa maambukizi linapokuja suala la Ebola.”
• Kumekuwa na ripoti za kushtusha za dhidi ya raia na wafungwa wa kivita wakati huu kukiwa na mashambulizi kamili ya kijeshi yanayofanywa na jeshi la Urusi huko Kyiv nchini Ukraine. Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu Shabia Mantoo amewaeleza waaandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo kuwa. “Zaidi ya wagonjwa 1,000 wamerekodiwa na wafanyakazi wetu wa Kamati ya wa Ufuatiliaji wa Haki za Binadamu kuanzia tarehe 24 Februari 2022 hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk ana wasiwasi mkubwa kwamba vitendo hivyo vya kuchukiza vinaendelea karibu katikati ya vurugu zisizoisha, na anahimiza vikomeshwe mara moja. Pia anatoa wito wa uchunguzi wa haraka, wa kina, na usio na upendeleo kuhusu madai yote ya unyanyasaji wa kingono, na kwa wale watakaopatikana na hatia wafikishwe mbele ya sheria.”
• Na, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limeonya kuwa msaada wa dharura unaotolewa kupitia mfumo wake wa pamoja wa kibinadamu nchini Sudan unaweza kuisha ndani ya wiki mbili zijazo kutokana na ukosefu wa fedha. IOM inasema inahitaji dola milioni 15 kuendeleza operesheni hiyo kwa kiwango cha chini kwa miezi 12, wakati watu milioni 8.6 bado wakiwa wakimbizi wa ndani nchini Sudan.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör
United Nations. Innehållet i podden är skapat av United Nations och inte av,
eller tillsammans med, Poddtoppen.