Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong anatarajiwa kwenda Ufilipino kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Asia Mashariki na Jukwaa la Kikanda la ASEAN.
Tume ya Dhamana na Uwekezaji ya Australia inasema imepata rekodi ya dola milioni 830 katika amri za adhabu za kiraia wakati wa Mwaka wa Fedha wa 2025-2026. Tume hiyo ilianzisha chunguzi zaidi ya 250, ambazo zilisababisha hatia 25 za jinai na watu 11 kuhukumiwa kifungo cha gerezani.
Karibu watu 930 wamefariki dunia kutokana na Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hii ikiwa ni kulingana na Wizara ya afya nchini humo. Vifo hivyo vimerekodiwa miongoni mwa visa 2,344 vya maambukizi vilivyothibitishwa hadi siku ya Jumamosi imesema wizara hiyo hii leo. Vifo vipya vilirekodiwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, idadi ya juu kabisa kuwahi kurekodiwa kwa siku moja.
Meli ya mafuta yenye bendera ya Tanzania imetekwa nyara na maharamia wanaoshukiwa kuwa wa Somalia katika pwani ya Yemen, vimebaini vyanzo vya usalama na maafisa wa eneo hilo kuhusu tukio hilo. Meli hiyo imehamishwa hadi majini katika eneo la Bari kaskazini mashariki mwa Somalia, kulingana na maafisa wa eneo hilo.