Send us Fan Mail

Katika episode hii tunazungumzia tofauti kati ya kumwamini Mungu na kuamini mbinu za kiroho. Mara nyingi waamini tunajikuta tukiegemea sana maombi, kufunga, ibada, na taratibu mbalimbali za kiroho kiasi kwamba tunasahau kuwa vitu hivi vilikusudiwa kutupeleka kwa Mungu — sio kuchukua nafasi ya Mungu mwenyewe.

Kupitia simulizi la Musa na mwamba, pamoja na mafundisho ya Yesu kuhusu mapokeo, tunatafakari namna ambavyo mbinu zinaweza kuwa muhimu kuliko uhusiano wa kweli na Mungu.

Je, bado tunamtafuta Mungu… au tumebaki kushikilia mifumo?

🎙 Mada hii ni mwaliko wa kurudi kwenye imani ya kweli, ushirika wa kweli, na kumtumaini Mungu zaidi ya tulivyozoea kufanya mambo ya kiroho.

#Faith #ChristianPodcast #Imani #RelationshipWithGod #ChristianLife #Jesus #SwahiliPodcast

Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör Tikvah. Innehållet i podden är skapat av Tikvah och inte av, eller tillsammans med, Poddtoppen.