Katika sehemu ya kwanza ya mfululizo wetu kuhusu AI na Ubunifu wa Injili, tunazungumza na Innocent Mwagilo — Music Producer, Songwriter na Sound Engineer.
Katika mazungumzo haya tunachunguza namna Artificial Intelligence (AI) inavyoendelea kubadilisha music production na ubunifu kwa ujumla. Je, AI ni tool nyingine tu kama tulivyozoea kutumia studio software, au imeanza kuchukua nafasi ya creativity ya mwanadamu?
Hili si mjadala wa kupinga au kuunga mkono AI.
Ni mazungumzo ya kutafuta hekima, kuelewa mabadiliko yanayotokea, na kujiuliza jinsi Wakristo wanavyoweza kuitumia teknolojia kwa namna inayomheshimu Mungu.
Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör
Tikvah. Innehållet i podden är skapat av Tikvah och inte av,
eller tillsammans med, Poddtoppen.