Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilisema kwenye taarifa yake ya Jumapili (Mei 31) kwamba, wagonjwa wengine zaidi wa Ebola wanatazamiwa kupona, hasa pale ugunduzi na matibabu yanapoanza mapema, wakati juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo hatari zikiongezeka.