Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mabadiliko ya tabianchi hayawaathiri watu wote kwa kiwango sawa.

Baadhi ya nchi zimejenga uchumi wao kwa miongo kadhaa kupitia matumizi makubwa ya nishati ya mafuta, huku nyingine zilizochangia kidogo katika uzalishaji wa gesi chafu zikikabiliwa na mafuriko, vimbunga, ukame, ongezeko la kina cha bahari na kupotea kwa njia za kujipatia riziki.

Hili ndilo kiini cha mjadala kuhusu haki na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ambao utafanyika kesho Jumatano . Lakini haki hiyo ina maana gani? Nani anapaswa kubeba gharama? Na kizazi kijacho kitaachiwa dunia ya aina gani?

Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

• Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umefungua pazia asubuhi ya leo saa za New York, Marekani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antono Guterres kupitia hotuba yake ambayo ni ya mwisho katika tukio hili amegusa mambo mengi miongoni likiwa kuhusu ushauri wake kuwa Umoja wa Mataifa unapaswa kufanya mageuzi katika Baraza la Usalama ili liakisi hali halisi ya ulimwengu wa leo na kuwa na uhalali pamoja na ufanisi unaohitajika kukabiliana na changamoto za sasa. • Tuondoke hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, ambako viongozi wa ulimwengu sasa wanaendelea kutoa hotuba zao nakupeleka mashinani hususan Nairobi, Kenya kusikia vijana wanataka nini. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör United Nations. Innehållet i podden är skapat av United Nations och inte av, eller tillsammans med, Poddtoppen.