Nafsi Yangu Ina Amani

Katika dunia ambayo inashangalia ukamilifu wa mwanaume, dunia ambayo bado haiko tayari kuzungumzia kwa kina juu ya afya ya akili ya mwanaume, dunia ambayo mwanaume anayepitia changamoto za afya ya akili bado anatengwa na kuonekana mtu asiyefaa kushirikishwa na jamii yake, Sunday Kapesi anapambana kubadilisha hayo.

Toka safari yake ya kuondokewa na baba yake mzazi, kuanza kuingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na kupata urahibu, kuweza kumuangalia mama yake na ndugu zake usoni na kukiri kwamba anahitaji msaada, na kuamua kwenda “rehab” ili aweze kupambana na urahibu huo, Sunday haachi simulizi yeyote kwenye mazungumzo haya.

Kama baba, kama mtoto, kama kaka, na kama mtu ambaye ana ndoto za kuisaidia na kuiokoa jamii yake, Sunday anaongea na sisi ni namna gani ni rahisi mno kwa mtu yeyote, hususani mwanaume kuingia kwenye urahibu, lakini pia anatutia moyo kwamba kila tatizo bado linauwezo wa kutatuliwa.

Ilimchukua muda kiasi gani kwa Sunday kupambania afya yake ya akili mpaka kufikia hatua ya kuweza kupata “amani kwenye nafsi yake”? 

Sikiliza kiundani mazungumzo haya ili na wewe uweze kufahamu kwamba haijalishi unapitia magumu kiasi gani, siku zote kuna suluhisho la unayopitia, na linaweza kuwa suluhisho bora ambalo litajenga zaidi afya yako ya akili na kukufanya uwe bora zaidi ya jana. Pambana kuipa nafsi yako amani

Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör Michael Baruti. Innehållet i podden är skapat av Michael Baruti och inte av, eller tillsammans med, Poddtoppen.