Baada ya kuzungumza naye katika sehemu ya kwanza, Bwana Ng’winula Kingamkono au maarufu zaidi kama #Unu wa Tunzaa anarejea tena katika Podcast yetu kwa sehemu ya pili na ya mwisho kwa sasa.

Safari hii Unu anaendelea kutupa ujuzi na uzoefu wake katika kuanzisha, kusimamia na kuendesha biashara ya “StartUp” yake Tunzaa.

Kumbuka, Unu hakuanzia hapa. Anaongea na Michael Baruti na Nadia Ahmed kuhusu maana ya mafanikio, maumivu aliyopitia, kitu anachojivunia na namna pia kwa upande mwingine kuwa baba kumekuja kuwa jambo bora na funzo bora sana kwake kama mwanaume, kaka, mtoto wa kwanza na zaidi ya yote kama mfanyabiashara. Na swala ambalo bado analilisitiza kwetu sote ni kuijua sifuri yetu. Je, wewe unaijua sifuri yako? Unajua ulipoanzia? Unajivunia safari yako? Sikiliza mazungumzo haya yenye mafunzo ya kutosha kwetu sote.

Podden och tillhörande omslagsbild på den här sidan tillhör Michael Baruti. Innehållet i podden är skapat av Michael Baruti och inte av, eller tillsammans med, Poddtoppen.